AN-NUUR 
Na.184 Ramadhan 1419, Januari 15 - 21, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma
 

KIKUNDI cha kina mama wa Kiislamu cha Bi Khadija cha mjini Dodoma kinatarajia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini. 

Bi Mwanahamisi Abdallah alimueleza mwandishi wa habari hizi kuwa mbali na kutoa msaada kwa wagonjwa, wataweka utaratibu wa kuwazungukia wagonjwa kuwafariji na kuwaombea dua. 

Hivyo, Bi Mwanahamisi amewaomba Waislamu wote wake kwa waume kushirikiana katika fikra hizi na kazi nzuri ambayo imeusiwa na Mtume (s.a.w.). 

Wakati huo huo, Imam wa Masjid Qubaa, Sheikh Abdallah Ally amewahusia Waislamu wa Dodoma na kwingneko kuwa wakarimu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa kufuturishana na kusaidiana. 

Sheikh Abdallah Ally amesema hayo katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani alipokuwa akiwahutubia mamia ya Waislamu waliohudhuria sala ya Ijuma. 

Sheikh Abdallah alisema tendo la kumfuturisha mtu aliyefunga lina ujira mkubwa sana mbele ya Allah (s.w.) na tendo hilo kila Muislamu analiweza kulifanya kadri ya uwezo alionao kwani alisema hata kumpa glasi ya maji au tende moja inatosha kupata ujira usiokadirika mbele ya Allah (s.w.). 

Aidha, Sheikh Abdallah amewahusia Waislamu kukithirisha sana kusoma Qur’an na kukhitimisha Qur’an nzima (juzuu 30) na wale ambao hawana kiwango kikubwa cha elimu inawatosha kusoma sehemu yoyote ya Qur’an anayo ifahamu kila mara, na kila siku. 

Nao waumini wa Masjid Qubaa wamechanga jumla ya shilingi 19,720 kwa wanafunzi wa Bihawana kama gharama za kununua futari na daku kwa wanafunzi 14 wa Kiislamu wa kidato cha nne ambao wapo shuleni wakisubiri kufanya mitihani yao. 


Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti

WAISLAMU wa kijiji cha Hamai, tarafa ya Goima wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma wamefikia kutoa wito kwa ndugu zao wa Kiislamu kuomba msaada wa hali na mali kumalizia jengo la Masjid Bilal na madrasa. 

Akitoa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi, Sheikh Ally Hassan Matundu amesema kuwa hatua waliyofikia inahitajika nguvu ya pamoja na Waislamu wengine waliyopo ndani na nje ya mkoa wa Dodoma ili kuweza kukamilisha awamu hiyo ya mwisho ya ujenzi. 

Mwandishi wa habari hizi alikutana na kamati kuu ya ujenzi na kuweza kupata kiini cha hali iliyofikia kuomba msaada huo. Mratibu wa ujenzi na shughuli za Da’awa Ustadh Rashid Salim Futa alisema, uchumi kwa kipindi hiki umekuwa mgumu sana hapo kijijini. 

Pamoja na kuwa asilimia 99.5 ya wakazi wa Hamai ni Waislamu, lakini hali ya njaa iliyoikumba wilaya ya Kondoa ikiwemo na kijiji cha Hamai imesababisha watu kujishughulisha na utafutaji wa riziki kwa familia zao. 

Aidha, Ustadh Futa alisema pia kuwa suala la kujenga Msikiti ni la kheri, hivyo Waislamu wa Hamai wangependa nao washirikishe ndugu zao kupata thawabu hizo. 

Jumla ya vifaa vifuatavyo vinahitajika kumalizia jengo hilo kama vile saruji tani 10, madirisha 11, mazulia, generator, rangi, dali (ceiling board) na vipaza sauti. 

Kwa upande wa Madrasati Bilal ambayo ujenzi wake umeunganishwa na Msikiti, wanahitaji vitabu, na mihutasari (syllabus). 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa 

Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd 

Ubungo yakumbwa na ukame 

Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema 

Dondoo za saikolojia 
Na. Abu Halima Sa Changwa 

Waislamu turejee kwa Allah 

MSADAT yazidi kutia moyo Tanga 

Mjue Usama bin Ladin 

MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI 

Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu 

Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii 

Hakuna Magharibi wala Mashariki: Uislamu ni ubinaadamu 
Na Abubakari S. Marwillo 

Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma mjini 
Na Abu Zuberi, Dodoma 

Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat - Tabata Kimanga 
Na B. Mwakangwale 

Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui 

Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana 

Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake 

Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma 

Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti 

Mnyororo wa imani-2 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Kutoka magazeti ya zamani: 
Wanaoshitakiwa kwa uhaini kortini leo 

Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa Kanisa la Walokole 
Na Mwandishi Wetu, Moshi 

Masjid Nurania yaswaliwa Ijumaa 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

Jabal Hira kutoa mafunzo ya Kompyuta Morogoro 
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Internet ni nini?] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Mashairi 

Chakula na lishe 
[Thamani ya mlo wa Uyoga] 
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita