Unapozungumza neno vijana kila mmoja kati yetu atatafsiri kwa maana tofauti lakini wote tutakuwa na ujumbe mmoja. Wapo watakaosema ni wale watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 45, wengine wangesema ni watu wale wenye uwezo wa kufanya majambo huku damu zikiwachemka na kadhalika. Ingekuwa vema kama ningelitoa fursa hii kwa vijana wenzangu kulitafsiri neno hili 'ujana'.
"Vijana msilale lale lale! Vijana msilale bado mapambano!" Lakini kwanini wawe vijana na wasiwe wazee au watoto? Huenda watunzi wa nyimbo hii walifahamu mengi juu ya vijana na uwezo wa vijana na katika utendaji wa kazi na ndio maana misingi yao ya hoja ilikita katika nukta hizi zifuatazo:
Moja, akili, akili ya kijana ni nyepesi kupokea mambo na kuyafanyia kazi, kwa sababu nafasi ya upokeaji na uchambuzi kiutendaji ni kubwa zaidi ukilinganisha na mtoto au mzee. Wazee wana tatizo la uzoefu (experience), anaweza kukataa jambo la kweli ati kwa sababu hakuwahi kuliona likitokea na ndio maana wajanja wakawatumia vijana katika kufanikisha mambo yao mbalimbali.
Mbili: Majukumu; kwa hali ya kawaida mzee mwenye watoto watano (5) wote wanasoma, wanahitaji mahitaji muhimu kama chakula, mavazi pamoja na malazi, ada ya shule na kadhalika ni vigumu kufikiria mabadiliko ya jamii na mantiki yake zaidi namna ya kuihudumia familia aliyonayo. Ndipo hapo vijana huchukua nafasi katika kufanya mabadiliko ndani ya jamii kulingana na uchache wa majukumu waliyonayo.
Tatu; nguvu na matumizi ya nguvu zao, ujana ndicho kipindi cha mabadiliko na nguvu nyingi kipindi ambacho mtu anakuwa na nguvu nyingi pamoja na afya bora, na nguvu hizi zinahitaji matumizi, zisipopewa matumizi bora basi zitatumika vibaya na ndio maana walezi wakachukua fursa hii kuwalea vijana ili kufikia malengo yao.
Nne, vijana ni rahisi kubadilika kulingana na ukweli uliowafikia (fact) ukilinganisha na wazee ambao wao wanakwazwa na uzoefu, majukumu na woga kulingana na hali zao walizonazo kiafya, hii pia iliwapa fursa walezi kutumia nyimbo hizi katika kutulea ili kufikia malengo yao.
Zaidi ya hayo, kwa sisi vijana wa Kiislamu hatuna budi kufahamu kuwa kila mmoja kwa wakati wake atasimamishwa katika mahakama ya Allah (s.w.) na miongoni mwa maswali atakayoulizwa ni ujana wako uliutumiaje? Kwa hivyo tujiandae kwa hilo.
Ndio maana ya kauli ya vijana msilale! Imeshika hatamu, ni kweli tumelala na wala hatujitambui tupo wapi, tunakwenda wapi na ipi hatma ya safari yetu, na ni nani dereva wa safari yetu hii.
Tukumbuke kuwa Mwenyezi Mungu ni mlinzi wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika mwanga. Lakini waliokufuru walinzi wao ni mashetani (twaghuti). Huwatoa katika mwangaza nakuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni huko watakaa milele. Ikiwa dereva wetu (muongozaji) ni Mwenyezi Mungu basi ni vema tujipongeze kwa hilo tena kwa vifijo na nderemo, aidha akiwa dereva wetu ni shetani (twaghuti) hatuna budi kujisikitikia kwani hatma ya safari yetu ni motoni".
"Bado mapambano!" Huu ni ujumbe wa pili wa nyimbo yetu. Na ndio fursa ya pekee ya kujiondoa katika gari hilo la motoni ikiwa tunauogopa moto wa Allah (s.w.). Swali la msingi la kujiuliza ni yapi mapambano hayo, lengo la maisha ndilo jibu la kitendawili hiki.
Ikiwa sisi vijana wa Kiislamu lengo letu ni kumwabudu Mwenyezi Mungu basi hapana budi kupambana na twaghuti (shetani).
Na ikumbukwe kuwa twaghut (shetani) anaipigania dini yake ili iwe juu ya Uislamu kwani, "Wale walioamini wanapigana katika njia (dini) ya Mwenyezi Mungu. Lakini wale waliokufuru wanapigana katika njia ya shetani (twaghuti). Basi piganeni na makafiri wa shetani. Hakika hila za shetani ni dhaifu". (4:78).
Mapambano yapo pande mbili tu, kupambana na dini ya Allah (s.w.) au kupambana na twaghuti (shetani), hivyo sisi kama vijana tuna njia moja kati ya hizo mbili na hakuna katikati katika njia hizo, kwa hiyo huree! Vijana tuchague njia ipi yatufaa.
"Na mnanini hampigani katika njia (dini) ya Mwenyezi Mungu (katika kuwaokoa) wale walo madhaifu..."(4:757).
Hata hivyo, kwanini tusipiganie njia ya Mwenyezi Mungu hali yakuwa mwongozo tunao, akili tunazo, nguvu tunazo na zipo? (Vitendea kazi vipo). Na ni vema pia tukawaidhika kuwa huu ni ukinzani wao wanavuta na sisi tunavuta ikiwa tutalegea au kuchoka tutavutwa na hatma yetu ni giza tena totoro.
Aidha, msingi mkubwa wa mapambano yetu ni utii kwa wale viongozi wetu tuliowachagua katika kuamshana, kujitambua na kutambua wapi tunatakiwa kwenda na namna gani tutafika huko kiutendaji tena kwa busara haswa.
Mwisho sina budi kutoa pongezi kwa vijana wa Kigoma, Sudani, Palestina, Talaban na kadhalika katika kuitikia wito wa vijana wa pangoni wa
kupigania dini ya Allah (s.w.)
(18:6-26).
--
|
|