Mapigano makali yaendelea Chechnya


MAPIGANO makali yamelipuka maeneo mbalimbali ya Chechnya ambayo Russia inadai kuyadhibiti.

Mashirika ya habari duniani jana yaliripoti kurejeshwa kwa miji ya Shaali na Argun chini ya udhibiti wa Russia.

Hata hivyo, taarifa za Wachechen zinafahamisha kuwa wapiganaji wao waliamua kuondoka katika miji hiyo baada ya kuyashambulia kwa ghafla majeshi ya Russia yaliyokuwa yakidhibiti miji hiyo. Taarifa nyingine zinadai habari zilizotolewa na Russia ni upuuzi mtupu.

Russia imekiri kupata hasara kubwa kutoka kwa wapiganaji wa Chechnya ambapo hadi jana zaidi ya askari wake 140 waliuawa na mamia wengine kujeruhiwa, vifaa kadhaa vya kijeshi vimeripotiwa kuharibiwa vibaya.

Wakati huo huo, katika hali iliyoonesha mtafaruku mkubwa katika jeshi la Russia kufuatia kipigo kutoka kwa Wachechen, Kaimu Rais wa Russia Vladmir Putin amemteua kamanda mpya mwingine kuongoza vikosi vya Russia.

Siku chache kabla ya uteuzi huo iliripotiwa kutokea mfarakano baina ya maafisa wa jeshi hilo ambapo baadhi waliwalaumu wengine kwa kutoa habari zisizo za kweli kuhusu hali ya uwanja wa vita.

Jeshi la Russia pia kufuatia kipigo cha ghafla katika miji ya Argun na Shaali wiki iliyopita limeanza kuwashambulia wakimbizi wanaovuka mpaka kuingia Angushatia.

Wavulana na watu wazima wanaume wamekuwa wakikamatwa kwa kile kilichodaiwa kuwa hujitia raia wa kawaida nyakati za mchana na lakini usiku hushiriki mapigano.

Mjini Moscow serikali ya nchi hiyo imeagiza idara ya usalama na shirika lake la ujasusi (KGB) kudhibiti mawasiliano binafsi ya simu, fax, E-Mail na barua za kawaida zinazoingia na kutoka nchini humo.

Serikali ya Russia imeamua kudhibiti habari zote kutoka uwanja wa mapambano.



Putin ajijenga kisiasa

KAIMU Rais wa Russia Vladmir Putin amepandisha malipo ya pensheni kwa waalimu na madaktari.

Wataalamu wa mambo ya siasa wameelezea hatua hiyo kuwa ni mojawapo ya kampeni za afisa huyo wa KGB kujijenga kisiasa wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu.

Uchaguzi mkuu wa Russia ambao huenda ukatawaliwa na mashushushu unatazamiwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu.

Mtu mwingine aliyejitokeza kupigana na Bwana Putin ametajwa kuwa ni afisa mkubwa katika shirika la kijasusi la nchi hiyo KGB.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook